Jumatatu 17 Agosti 2026 - 10:00
Mashia Wakamatwa Kisa Kuomboleza Kuuwawa Kishahad Imam Ridha (as)

Hawza/ Mamlaka za usalama za Bahrain katika wiki za hivi karibuni zimekamata makumi ya raia wa Kishia, wakiwemo baadhi ya wanazuoni na waombolezaji wa kidini.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mamlaka za usalama za Bahrain katika wiki za hivi karibuni zimechukua hatua ya kukamata makumi ya raia wa Kishia, wakiwemo baadhi ya wanazuoni, waombolezaji na wahutubu, kwa sababu ya kufanya shughuli zao za kidini.

Vyanzo vya wananchi vilieleza kuhusu kukamatwa kwa khatibu wa Husseini na mwalimu wa Hawza, Sheikh “Jaafar al-Sitri al-Amjadi”, ambaye baada ya kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa kiusalama, alikuwa amejiandaa kufika mbele ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka siku ya Jumanne, tarehe 20 Mordad 1405 (11 Agosti 2026).

Kamatakamata imeendelea kupitia miito ya kiusalama, na kuwahusisha raia wafuatao: “Saeed Akbar al-Mulla, Ali al-Qassab, Ali Saeed, Hussein al-Arab, Hussein Abd al-Ilah, Muhammad Amin, Sayyid Hashim Ibrahim, Hamza Saeed Zuhair, Ahmad Yasin Zuhair, Sayyid Abbas Sayyid Tahir na Ridha Hussam.”

Vyanzo hivyo viliongeza kuwa: Baada ya kuwaita kwa ajili ya kuhojiwa, mamlaka ziliwakamata raia watatu kutoka “mji wa Samaheej” kwa sababu ya kushiriki katika shughuli za maombolezo usiku wa kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Imam Ali bin Musa al-Ridha (as), ambao ni: “Abdullah Sabt, Abbas Abdullah, Hussein Shamsan na Ali Makki”; vilevile raia “Sayyid Ali Sayyid Mazin” alikamatwa alipokuwa akipita katika kituo cha mpaka cha “King Fahd Causeway”, na raia “Hassan Yusuf al-Asfour” alikamatwa alipokuwa akisafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bahrain.

Katika tukio hili, mamlaka pia ziliwalenga watu watatu waliokuwa na majukumu katika Husayniyah, wakiwemo raia wawili, “Muhammad Hassan Jassim al-Nakkal na Sayyid Abdullah Hashim al-Khurajani”, kutoka “Jumuiya ya Sitra al-Kharija”, pamoja na raia “Ahmad Abd al-Nabi Zayer”, miongoni mwa wasimamizi wa “Husayniyah Ansar al-Adalah” katika mji wa Al-Diraz.

Mambo hayo pia yalihusisha uvamizi uliofanywa katika maeneo kadhaa na mawakala wanaohusishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain, ambao ulisababisha kukamatwa kwa raia “Younis Ahmad Hammad, Abdullah Fadhil al-Daqqaq, Hassan Abd al-Amir na Isa Abbas”; wakati huo huo, kupitia miito ya kuhojiwa kiusalama, raia wafuatao pia walikamatwa: “Hassan Ali al-Tajir, Muhammad Abd al-Wahhab Habib, Sayyid Saleh Nizar al-Alawi, Yusuf Mohsen al-Mughni, Zuhair Jaafar Abu Ruwais, Hussein Abdullah Juma, Nasrullah Mansour (kijana) na Jaafar al-Zaki.”

Mamlaka za usalama za Bahrain, baada ya kuanza mashambulizi ya Marekani na Wazayuni dhidi ya Iran, zimewakamata mamia ya raia, wakiwemo wanawake, watoto na wanazuoni wa dini. Zimetekeleza aina mbaya zaidi za mateso dhidi ya waathirika wao; tukio la hivi karibuni likiwa ni kifo cha kishahidi cha raia wa Kishia “Sayyid Muhammad Mohsen al-Mousavi” chini ya shinikizo la mateso. Tukio hilo lilitokea baada ya mashambulizi ya kichochezi ya kimadhehebu kwenye mitandao ya kijamii na madai ya kuwataka kutekeleza hukumu za kunyongwa kwa misingi ya misimamo yao ya kisiasa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha